Mratibu Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akizungumza na baadhi ya watumishi wa shule ya sekondari Jamsi Sangu (hawapo pichani ) juu ya namna ya kujiunga na fao hilo kabla ya kufanyika kwa zoezi la makabidhiano ya hundi kwa Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo
yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake ambaye alikuwa mteja wa taasisi hiyo kufariki dunia.,
yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake ambaye alikuwa mteja wa taasisi hiyo kufariki dunia.,
(Picha zote Emanuel Madafa Jamiimoja blog Mbeya .
Alpha Akimu Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini akizungumza katika hafla hiyo . |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu (3,000,000), Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Jamsi Sangu iliyopo Vwawa Mbozi Mkoani mbeya , ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake kufariki dunia ambaye alikuwa Said mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao .
Akizungumza katika makabidhiano hayo wilayani Mbozi mkoani Mbeya , Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, amesema mzazi wa mwanafunzi huyo Jaqline Ndyamkama
ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo sasa imemnufaisha mtoto wake.
ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo sasa imemnufaisha mtoto wake.
Amesema fao hilo la elimu limekuwa msaada mkubwa kwa wategemezi mara baada ya wazazi kufariki dunia kwani imechangia kwa kiwango kikubwa wategemezi hao kukamilisha ndoto zao kwa uhakika zaidio licha ya kufiwa na wqzazi wao.
“Naomba Watanzania wote waweke utaratibu wa kujiunga na bima hii ambayo malipo ya kila mwezi kwa fao la Bronze ni Sh 3500 tu, huku mafao yake yakiwa ni Sh 1,800,000, huku Makato ya bima ya Silver yakiwa ni Sh 7,000 na fao lake ni Sh 3,700,000 na Gold akilipwa mteja Sh 7,500,000 wakati makato yake yakiwa ni Sh 12,000 tu kwa mwezi,” alisema Ruth.
Naye Jaqline ameishukuru taaasisi hiyo ya Bayport kwa huduma zao nzuri, huku akisema mafao ya mama yake yatachangia kwa kiasi kikubwa kukamilisha ndoto zake kwani bado anasafari ndefu katika kufikia malengo ya kielimu huku pia akiwataka wazazi na walezi kujiunga na utaratibu huo.
Aidha kwa upande wake bibi mlezi wa Jaqline Ndyamkama ,Angelika Geka , amesema hajawahi kuona taasisi yenye huduma nzuri kama Bayport Financial Services, hasa baada ya kuhakikishiwa malipo ya mafao hayo ambayo tayari yamekwisha fanyika malipo ya ada ya mjukuu wake bila usumbufu wowote, jambo ambalo ni nadra kwa taasisi nyingi nchini.
Aidha, utaratibu wa malipo ya huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao umepangwa kulipwa kila mwaka, ili kuhakikisha kuwa mafao hayo yananufaisha walengwa, hususan kwa wale wanaoendelea na masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini.
Comments