MAMA SALMA AWASILI NAIROBI KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA AFRIKA KUHUSU KANSA YA MATITI,SHINGO YA KIZAZI NA TEZI DUME.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Esther Wanjiru anayelelewa katika Kituo cha watoto cha Mama Ngina huko Nairobi muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya tarehe 19.7.2015. Mama Salma yupo nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa Barani Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta huko Narobi tarehe 19.7.2015. Aliyesimama nyuma kulia ni Mheshimiwa Korere Sarah, Mbunge wa Jimbo la Laikipya katika Mkoa wa Rift Valley aliyekuja kumpokea rasmi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na Mheshimiwa Korere Sarah wakipata mapumziko mafupi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea hotelini walikopangiwa.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Ndugu John Haule akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Intercontinental iliyoko Nairobi tarehe 19.7.2015 kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wake wa Marais wa Afrika utakaozungumzia magonjwa ya kansa ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margret Kenyatta wakati wa tafrija ya kuwakaribisha kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume. Tafrija hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Madame Lordina Draman Mahama, Mke wa Rais wa Ghana wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi tarehe 19.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Niger Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Africa wanaokutana Nairobi kuzungumzia kansa ya matiti, kizazi na tezi dume.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Namibia Mheshimiwa Monica Geingob wakati wa tafrija kwa wajumbe wa mkutanon wa 9 wa wake wa Marais wa nchi za Afrika tarehe 19,7.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI
Comments