Sunday, July 19, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA BARAZA LA SIKUKUU YA EID EL- FITRI KITAIFA MKOANI GEITA.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Barala la Sikukuu ya Eid El- Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana ya Nyankumbu, mkoani Geita Julai 18, 2015.
Picha na OMR
4
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Baraza la Sikukuu ya Eid El- Fitri, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bi Fatma Maswi, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia katika Baraza hilo lililofanyika Kitaifa Mkoani Geita Julai 18, 2015.
5
Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia katika Baraza hilo.
6
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) Suleiman Lolila, akizungumza, kabla ya kumkaribisha Kaimu Mufti.
7
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bi Fatma Maswi, akizungumza kuwakaribisha wageni katika hafla hiyo ya Baraza la Sikukuu ya Eid El- Fitri.
8
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Sheikh  Haruna Abdallah Kichwabuta, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal kuhutubia.

No comments: