MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO MAALUM “CWL-INTERNATIONAL WOMEN OF EXCELLENCY AWARD FOR LEADERSHIP”

1
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Profesa Sulochana Nair ,Makamu na Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Binary kilichoko Kuala Lumpur nchini Malaysia mara baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.7.2015. Aliyesimama kushoto ni Profesa Joseph Adaikalam, Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo hicho. 
2
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea TUZO maalum ya “ CWL International Women of Excellency Award for Leadership” kutoka kwa Profesa Joseph Adaikalam, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Chuo Kukuu cha Binary kilichoko nchini Malaysia kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika maendeleo ya wanawake nchini Tanzania na Afrika tarehe 24.7.2015. Aliyesimama (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima, akifuatiwa na Profesa Bulochana Nair na Kulia ni Profesa Datin Rohini Devi wa Chuo Kikuu cha Binary.
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Profesa Joseph Adaikalam (kulia) Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa  Chuo Kikuu cha Binary kilichoko Kuala Lumpur nchini Malaysia na kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Sulochana Nair tarehe 24.7.2015.
4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Binary kwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz  Mlima tarehe 24.7.2015.
5
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akishuhudia utiaji saini  (MoU) wa fursa za Binary First Lady of Tanzania Scholarship kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu Cha Binary. Wanaotia saini ni Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA na Profesa Joseph Adaikalam, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Binary cha nchini Malaysia tarehe 24.7.2015. Kupita makubaliano hayo Chuo Kukuu cha Binary kitatoa nafasi 10 za shahada za uzamili.
6
Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Binary Profesa Joseph Adaikalam akibadilishana hati za makubaliano (MoU) na Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishuhudia.
78
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba mara baada ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya “ CWL International Women of Excellency Award for Leadership’ na Chuo Kikuu cha Binary kilichoko nchini Malaysia tarehe 24.7.2015. 
910
Baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu cha Binary na wqageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya tuzo na utiaji saini ya Makubaliano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Binary tarehe 24.7.2015 huko Kuala Lumpur nchini Malaysia.
PICHA NA JOHN LUKUWI.

Comments