MUSTAFA PANJU ACHUKUA NA KURUDISHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI AAHIDI UMOJA NA MAENDELEO
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano fomu ya kuwania kinyang’anyiro hicho baada ya kuchukua fomu hiyo jana na kurejesha huku akisisitiza kuwa endapo atafanikiwa kupitishwa na chama hicho au laa atashirikiana na wananchi pamoja na wanaCCM katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo ambalo lipo mikononi mwa chama cha Demokrasia na maendeleo( CHADEMA).
Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akionyesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano jana katika ofisi za CCM wilaya
Hapa Mustafa Panju akiandika jina lake katika fomu yenye majina ya waliokuja kuchukua fomu kupitia chama hicho kwa Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ,kushoto ni mke wake aliyemsindikiza kuchukua fomu
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano akionyesha kadi ya mgombea ubunge kupitia chama cha CCM Mustafa Panju
Comments