Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi waliokamatwa pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya operesheni katika mapori(Picha na Victor Masangu)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi waliokamatwa pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya operesheni katika mapori(Picha na Victor Masangu)
………………………………………………….
VICTOR MASANGU, PWANI
KUFUATIA kukithiri kwa wimbi la matukio ya uharifu pamoja na kuvamia vituo vya polisi Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa wa ujambazi 27 pamoja na risasi 153,bunduki 2 mabomu 3 ambavyo walikuwa wakivitumia katika matukio ya uharifu.
Akizungumza na wa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wamejificha.
Kamanda amesema kwamba wameamua kufanya operesheni hiyo kutokana na kuongezeka kwa uharifu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na kuwakamata watuhumiwa hao ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali ikiwemo visu mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.
Aidha Kamanda huyo amebainisha kwamba katika zoezi hilo pia waliweza kukamata madawa ya kulevya aina aya bangi gunia 18 na mirungi kilo 124,lita 88 za pombe ya moshi pamoja na mitambo yake mitatu ya kutengenezea noti bandia 370 na meno ya tembo.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo amesema kwamba wanafunzi wawili wa familia moja katika shule ya msingi mgogodo iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamepoteza maisha baada ya chumba chao walichokuwa wamelala kuteketea kwa moto na kwamba chanzo cha moto huo ni kibatali.
Mkoa wa pwani umekuwa na matukio ya uharifu mbali mbali ikiwemo kuvamiwa kwa vituo vya polisi ikiwemo kituo cha Kimazichana Wilayani mkuranga ,Ikiwiriri ,kituo kidogo cha mloka,pamoja na tukio la kufanya jaribio la kutaka kuvamia kituo cha polisi Kibiti vyote vilivyopo Wilayani Rufiji.
Comments