Tuesday, July 21, 2015

RAIS KIKWETE APOKEA HUNDI YA BIMA YA MAISHA

mail.google.com
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hundi ya malipo ya Bima ya Maisha(Flexi Provider) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa(National Insurance Corporation of Tanzania Limited) NIC  Bwana  Sam Kamanga ikulu jijini Dar es Salaam julai 21, 2015.
Picha na Freddy Maro
…………….
Akimkabidhi hundi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Tanzania Limited  (NIC) Bw. Sam Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye.
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na Bima.
B

No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...