Monday, July 20, 2015

KADA WA CCM ASSENGA ALITAKA JIMBO LA KILOMBERO

 Kada wa CCM, Abbakar Assenga akitangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, mbele ya umati wa wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara.
 Msanii wa muiziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, akizungumza na umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Kada wa CCM, Abubakari Assenga (kushoto) aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Kilombero kwenye mkutano huo
 Ali Kiba akiwapa hi, umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Assenga kutangaza nia ya kuwania ubunge, jimbo la Kilombero mkoani Morogoro,  kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara, baada ya mechi ya fanali ya Kombe la Assenga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Asante Afrika, Ifakara
 Mchezaji wa timu ya Lumemo Ashir Mtenge (kushoto), akipambana na mchezaji wa Kining’ina  Juma Ngulukila, timu hizo zilipoemnyana katika mechi ya fainali ya Kombe la Assenga, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara mkoani Morogoro.  Kining’ina iliibuka bingwa wa kombe hilo baada ya kuicharaza Lumemo mabao 6-0 katika mechi hiyo.
 Mchezaji wa timu ya Lumemo Ashir Mtenge (kushoto), akipambana na
mchezaji wa Kining’ina  Juma Ngulukila, timu hizo zilipoemnyana katika
mechi ya fainali ya Kombe la Assenga, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Kining’ina, Ifakara mkoani Morogoro.  Kining’ina iliibuka bingwa wa
kombe hilo baada ya kuicharaza Lumemo mabao 6-0 katika mechi hiyo.
 Wachezaji wa Kining’ina wakishangilia bao la tano dhidi ya Lumemo wakati wa mechi hiyo
 Msanii wa muziki, Ali Kiba, akifuatilia mechi ya Lumemo na Kining’ina ya
fainali ya Assenga Cup kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara, mkoani
Morogoro, mwishoni mwa mechi hiyo, kada wa CCM, Aboubakar Assenga
alitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero
 Ali Kiba na Assenga wakiwa kwenye mechi hiyo
 Mashabiki wakiwa kwenye mechi hiyo ya fainali ya ssenga Cup, kenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara mkoani Morogoro.
 Wachezaji wa timu ya Kining’ina wakijinasibu baada ya kuibuka mabingwa wa Assenga CUP kwenye mechi hiyo
Wananchi wakishangilia wakati Kada wa CCM, Aboubakar Assenga alipokuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara.
 Ali Kiba akimpa zawadi mchezaji bora katika mechi hiyo
Aboubakar Assenga akikabidhi zawadi ya pea moja ya jenzi, alipogawa jozi moja ya jezi kwa timu zote zilizoshiriki michuano ya Assenga Cup
Ali Kiba akitoa zawadi  kwa nahodha wa timu ya Lumamo Cup, Hamza Ali baada ya timu hiyi kuibuka mshindi wa pili katika fainali za kombe la Assenga.
Ali Kiba akikabidhi zawadi ya kitita cha fedha kwa nahodha wa timu ya Kining’ina, Mohammed Abeid, baada ya timu hiyo kuibuka bigwa wa michuano ya Assenga, baada ya tmu hiyo kuizaba mabao 6-0 timu ya Lumamo katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kining’ina, Ifakara. Kushoto ni Kada wa CCM Aboubakar Assenga ambaye baadaye alitangaza nia kuwania ubunge jimbo
la Kilombero
Msanii Ali Kiba akiwasili kwenye Uwanja wa Michezo, kumpiga tafu Kada wa CCM, Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Kilombero, katika mkutano uliofanyika Mang’ula mkoani Morogoro.
Msanii Alikiba akinena na wananchi alipompa tafu, Kada wa CCM, Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo
la Kilombero, katika mkutano uliofanyika Mang’ula mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mkutano huo, kushoto ni Zainabu Bakari kutoka Umoja wa Vijana wa CCM.
Mtoto na karanga zake akiwa kwenye mkutano huo
Alikiba akiwasha moto kwa kuwashindanisha vijana kucheza muiziki wake kwenye mkutano huo
Baada ya kunogewa, Ali Kiba akaamua na yeye kusakata muziki na vijana hao aliokuwa akiwashindanisha.
Mama akishangilia kwa nguvu zake zote, Kada wa CCM, Abubakar Assenga alipokuwa akitangaza nia kuuwania ubunge jimbo la Kilombero katika mkutano huo uliofanyika Mang’ula.
Vijana wakiwa wamepanda kwenye mti kuhakikisha wanamuona Assenga wakati akitangaza nia kwenye mkutano huo
Assenga aakiwasalimia wananchi alipowasili katika mkutano wke wa kutangaza nia ya kugombea ubunge, uliofanyika Mang’ula
Kada wa CCM, Abubakar Assenga akiwahutubia wananchi alipotanagaza nia kuwania ubunge jimbo la Kilombero, katika mkutano uliofurika wananchi hao katika eneo la Mang’ula
Assenga akishauriana jamabo na Mweneyekiti wa CCM
Assenga akishauriana jambo na Kijana wa CCM Zainabu bakari
Abubakari Assenga, ambaye alikuwa akitangaza nia kuwania Ubunge jimbo
la Kilombero, akiwa na Ali Kiba jukwaani mwishoni mwa mkutano huo uliofanyika Mang’ula mkoani Morogoro. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO, KILOMBERO

No comments: