JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (United Nations) Mhe. Ban Ki-moon tarehe 16 Machi, 2015 alimteua
Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kuwa
Mwenyekiti wa jopo huru la wataalamu wa kutafuta ukweli zaidi juu ya kifo cha
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hayati Dag Hammarskjöld,
kifo hicho kilichotokea kwenye ajali ya kusikitisha ya ndege mnamo tarehe 17-18
Septemba, 1961 maeneo ya Ndola, Zambia wakati akitafuta suluhu ya mgogoro wa
wakati wa vita vya Nchi ya Congo (DRC). Pamoja naye jopo hilo
lilikuwa na wajumbe wawil Bw. Kerryn Macaulay wa Australia and Henrik Larsen wa
Dermark. Kazi hiyo iliyochukua miezi
mitatu imekamilika na kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu, Ban Ki-moon ambaye pia ameiwasilisha kwa Rais
wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili ya ripoti hiyo inapatikana kwenye
tovuti ya Umoja wa Taifa ya http://www.un.org/dous/journal/asp/ws.asp?m=a/70/132.
Aidha taarifa ilitolewa kwenye vyombo vya habari ya tarehe 6 Juni, 2015, inapatikana kupitia tovuti
http://www.un.org/press/en/2015/sgsm/6916.doc.htm
Mahakama, tunachukua
fursa hii kumpongeza Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji
Mkuu kwa uwakilishi wa Mahakama na Nchi
yetu na kazi iliyotukuka na kumtakia heri na mafanikio zaidi.
H. A. Kattanga
MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA
MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA
Comments