Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda akifungua rasmi mkutano wa Marais wastaafu wa Afrka AFRICA LEADERSHIP FORUM unaofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Mkutano huo unaojumuisha marais wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania , Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Festus Mogaye wa Botswana, Bakili Muluzi wa Malawi na Jerry Rowlings wa Ghana unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika bara la Afrika na Changamoto zinazokabili barahilo na umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Marais wastaafu Bakili Muluzi wa Malawi kulia na Jerry Rawlings wa Ghana wakiwa katika mkutano huo.
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kushoto na Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu Mstaafu wa AU na Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
Gavana wa Benki KuuProf. Beno Ndulu wa tatu kutoka kulia na wageni mbalimbali wakihudhuria katika mkutano huo.
Marais wastaafu kutoka kushoto ni Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia,Benjamin Mkapa wa Tanzania na Festus Mogaye wa Botswana wakifuatilia mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin Mkapa akitoa mada katika mkutano huo.
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda kulia akiwa katika mkutano huo pamoja na marais wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu wa Nigeria Mh. Olusegun Obasanjo.
Comments