LOWASSA AHAMIA RASMI CHADEMA, UKAWA WAFURAHIA

Edward Lowassa akiwapungia mkono makada wa vyama vya UKAWA na CHADEMA baada ya kuwasili ukumbini.
Edward Lowassa akiwapungia mkono makada wa vyama vya UKAWA na CHADEMA baada ya kuwasili ukumbini.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (kushoto) akiteta jambo na Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho leo.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (kushoto) akiteta jambo na Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho.
Edward Lowassa akizungumza na Prof. Ibrahim Lipumba (kulia).
Edward Lowassa akizungumza na Prof. Ibrahim Lipumba (kulia).
Edward Lowassa akitangaza kuihama CCM na kujiunga na CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA.
Edward Lowassa akitangaza kuihama CCM na kujiunga na CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA.
Freeman Mbowe (kushoto) akimkabidhi kadi ya CHADEMA, Edward Lowassa
Freeman Mbowe (kushoto) akimkabidhi kadi ya CHADEMA, Edward Lowassa
Lowassa, na mkewe pamoja na meza kuu wakionesha kadi za CHADEMA.
Lowassa, na mkewe pamoja na meza kuu wakionesha kadi za CHADEMA.
Meza kuu ya mkutano huo ikifurahiya jambo.
Meza kuu ya mkutano huo ikifurahiya jambo.
Baadhi ya viongozi na makada wa vyama vinavyounda UKAWA na viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano wa kumtambulisha Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.
Baadhi ya viongozi na makada wa vyama vinavyounda UKAWA na viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano wa kumtambulisha Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.
Baadhi ya viongozi na makada wa vyama vinavyounda UKAWA na viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano wa kumtambulisha Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.
Baadhi ya viongozi na makada wa vyama vinavyounda UKAWA na viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano wa kumtambulisha Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.
ALIYEKUWA Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Edward Ngoyai Lowassa na kada mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akiacha historia ya pekee nchini Tanzania.
Lowassa ametangaza uamuzi huo leo alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, baadhi ya viongozi wa CHADEMA na viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA) katika Hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach Hoteli iliyopo eneo la Kunduji jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo uliokuwa na ulinzi mkali kiusalama ambapo kila aliyeingia kwanza alipekuliwa na kisha kuhakikisha jina lake lilitumwa mapema kwamba anaalikwa kushiriki mkutano huo na si vinginevyo na watu ambao hawakutambulika wala kualikwa katika mkutano huo hawakuruhusiwa kuingia ukumbini. Ndani ya ukumbi pia hakukuwa na ruhusa kusimama zaidi ya waandishi wa habari wapiga picha ambao waliruhusiwa kutokana na kazi yao.
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na viongozi wa juu wa vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, NLD pamoja na wenyeji CHADEMA viongozi wa vyama hivyo ambao ndio wanaounda ushirikiano wa UKAWA walionekana kumuunga mkono Lowassa wazi wazi kugombea nafasi ya urais kupitia UKAWA kwa mgongo wa chama cha Chadema. Hata hivyo hawakutamka moja kwa moja kwamba tayari wameridhia Lowassa kusimama katika kinyang’anyiro cha urais kwa mwamvuli wa UKAWA.
Akizungumza Lowassa alisema azma yake ya kusimama kama mgombea urais wa Tanzania ili aweze kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya nchi na kuondokana na umasikini upo pale pale licha na jina lake kukatwa kinyemela na Chama Cha Mapinduzi Dodoma. Alisema mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa katiba na taratibu za uchaguzi wa CCM, huku ukiwa na upendeleo mkubwa na kuonesha chuki dhidi yake.
Alisema kikatiba ya CCM kamati ya maadili iliyokata jina lake na majina mengine haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi lakini ilifanya hivyo. “…Kikatiba kamati ya maadili ya CCM si chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea Urais kupitia CCM. Kilichotokea Dodoma ni kupora madaraka ya Kamati Kuu na kukiuka Katiba ya CCM,” Aidha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu viliitishwa na kuburuzwa ili vitekeleze azma ya watu binafsi pasipo kujali demokrasia, Katiba, Kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM,” alisema Lowassa.
Aliongeza kuwa aliwekewa mizengwe na kuzushiwa majungu na uongo mwingi kuhakikisha jina lake halifikishwi ndani ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu na kujadiliwa licha ya kuwa ndiyo mgombea pekee aliyekuwa akiungwa mkono na wanachama na wananchi ukilinganisha na wenzake wote.
Alisema njama ndani ya CCM dhidi ya mpango wa kuchafua jina lake si jambo jipya kwani imekuwepo mikakati hiyo ambayo baadhi ya vijana walitumika kulichafua jina lake na kuzusha uwongo ambao baadaye walizawadiwa madaraka makubwa.
“…Naamini sikutendewa haki katika mchakato mzima wa kupendekeza majina na kuteuwa mgombea wa Urais wa CCM. Nilinyimwa haki yangu ya msingi ya kusikilizwa na kuchaguliwa kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nikiendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu,” alisema na kuendelea…
“..Nidhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema IMETOSHA na SASA BASI! Kama baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere alivyosema, CCM siyo baba yangu wala mamayangu na Kwamba kama Watanzania hawapati mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sasa tuyatafute mabadiliko nje ya CCM,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.
Alisema ameitikiwa wito wa UKAWA na kuingia CHADEMA ili kushirikiana na umoja huwo kuleta mabadiliko ya kweli ya taifa, uamuzi ambao ameufanya baada ya kufikiria vya kutosha na kujiridhisha kuwa ndani ya UKAWA wanaweza kushinda Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba 2015 na kuleta babadiliko hayo ya kihistoria. Aliwaomba Watanzania wenye nia ya kweli ya kuleta maendeleo na demokrasia ya dhati kujiunga na umoja huo ili kushirikiana katika safari mpya ya kuinusuru nchi.
Uamuzi wa Lowassa kuihama CCM na kujiunga na upinzani ni historia ya kwanza kwa kiongozi aliyeshika nyazifa za juu za nchi ya Tanzania huku akiwa na ushawishi mkubwa wa Watanzania kujiunga na upinzani akiwa na mtazamo wa kuleta mabadiliko ambayo anaamini hayapatikani ndani ya chama hicho. Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu, Waziri na kushika nafasi anuai, kada mkubwa ndani ya CCM anakuwa ni kiongozi anayeacha historia kwa uamuzi wake.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Comments