JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO

Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake, Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini, Joel Makwaia akizungumza katika mkutano wa Chadema alipoalikwa kukiwakilisha chama chake.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Moshi mjini,Leonard Buberwa akizungungumza akati wa mkutano wa kumpata mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
Watia nia katika nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini,Basil Lema,(kushoto) Jafary Michael (katikati) na wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko  wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza.
Mbunge wa iti maalumu,Chadema,Lucy Owenya alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge aliyejitokeza kutetea kiti chake.
Wajumbe wa mkutano wakishangilia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Msimaizi wa Uchaguzi ,katibu wa baraza la wanawake mkoa wa Kilimanjaro ,Helga Mchomvu akitangaza matokeo katika uchaguzi huo ambao mgombea Basil Lema aliamua kujitoa kabla ya kura kupigwa.
Mtia nia aliyetangazwa mshindi Jafary Michael akiwa na mkewe katika ukumbi wa Umoja Hotel ambako uchaguzi huo ulifanyika.
Mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo aliyepata kura 9 ,Elikunda Kipoko akizungumza na kuwashukuru wajumbe kwa wale waliompigia kura .
Jafary Michael aliye chaguliwa na Chadema kupeperusha Bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba katika kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Michael aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,akimtambulisha mkewe mbele ya wapiga kura.
Mgombea wa nafasi ya viti maalumu ,Lucy Owenya akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumuamini na kumchagua tena kupeperusha bendera ya chama hicho kupitia viti maalum.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema aliyekuwa miongoni mwa wagombea kabla ya kujitoa akizungumza katika mkutano huo mara baada ya Jafary Michael mkutano huo kupitisha jina lake kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama hicho katika jimbo la Moshi mjini.  

Comments