Thursday, July 16, 2015

DC MAKONDA AKUTANA NA VIJANA WASIO NA AJIRA NA KUWAUNGANISHA, KUBUNI MIRADI YA KIUCHUMI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA

????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana  ambao hawana ajira  wenye elimu tofauti  katika viwanja vya Leadres jijini Dar es salaam, ambapo amekutana na vijana hao  ili kuzungumza nao kwa ajili ya kutatua tatizo lao lao la ajira . 

DC Makonda amesema lengo la kuwaita vijana hao ilikuwa ni kuwakutanisha  wafahamiane na wabadilishane mawasiliano lakini pia wataunda vikundi vyao kulingana na taaluma zao na kila kundi litaandika miradi ipatayo mitano ili tuweze kuifanyia kazi kwa kuwatafutia mitaji au ufadhili baada ya miradi yao kubuniwa ,

Ameongeza kwamba mpango huu utapunguza vijana kukaa bila kazi na kuingia katika vishawishi vya mimba kwa wasichana na na matukio yasiyo mema katika jamii. kama vile uhalifu na mengine mengi.

Lakini pia amesema kuna makampuni mengi yameahidi kuchukua vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwani kwa kuwaunganisha vijana hao litakuwa ni jambo rahisi kupata wafanyakazi wa kuajiri , ikiwa ni pamoja na kuchukua vijana watakaofanya kazi kwa kujitolea na baada ya kuonyesha uwezo kazini wao wataajiriwa na mashirika au taasisi husika.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na vijana hao kwenye viwanja vya Leaders
????????????????????????????????????
Baadhi ya vijana wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????

????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha Chanel Ten.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...