Tuesday, July 21, 2015

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

IMG_9354Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
IMG_9341Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
IMG_9348
IMG_9317Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.

No comments:

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefan...