Wednesday, December 02, 2015

WACHINA WAONYESHA UTAMADUNI WAO TANZANIA

ci1Kikundi cha wanamuziki kutoka China kikitumbuhiza wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa China hapa nchini.
ci2Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Di Yang akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci3Msanii wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Yang Jing akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
ci4Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa kundi la Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China. Kundi hilo linaundwa na wanazuoni na watafiti wa muziki wa asili nchini China.
Picha na Frank Shija, WHVUM
…………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho
Maonesho ya utamaduni wa watu wa China yalifanyika jana usiku maeneo ya Makumbusho ya TaifaJijini Dar es salaam baada ya ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China uliofanyika mchana.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa kituo hicho cha Utamaduni wa watu wa ChinaTanzania Bwana GAO Wei ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni waalikwakuangalia utamaduni wa wachina kupitia muziki wao.
Hafla hiyo ilipambwa na wanamuziki mahiri wa kundi la watafiti wa muziki wa asili linaloitwa Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China kilichopo Beijing. 
Wanamuziki hao walianza kwa kupiga vyombo vyao vya muziki kwa pamoja bila kuimbachochote na baadae kila mmoja wa wanamuziki hao alipiga chombo kimoja cha muziki ilikuwaonyesha wageni waalikwa sauti na mdundo wa kila chombo cha muziki.
Mwishoni walipiga vyombo vyao kwa pamoja kwa kupiga mapigo ya wimbo wenye asili yakitanzania unaoitwa ‘Malaika Nakupenda’.
Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania ndio kituo cha kwanza kufunguliwa kwa Afrika Mashariki. Kimefunguliwa rasmi jana saa nne kamili asubuhi.Kituo hicho kipo Barabara ya Hassan Mwinyi maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.

No comments: