Friday, December 11, 2015

MILLICOM KUANZA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WAKE WA UWEKEZAJI KWA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL TANZANIA

 Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel Bi Rachel Samren, akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya mikakati ya Millicom katika kuiboresha kampuni ya Zantel.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom upande wa Africa, Cynthia Gordon, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi juu ya mipango ya kampuni yake ikiwamo kuzindua mtandao wa 4G upande wa Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Zantel katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel akijibu maswali ya waandishi katika mkutano huo. Kushoto kwake ni Rachel Samren, Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na kulia ni Cynthia Gordon, Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.


Mwenyekiti wa Bodi, Rachel Samren akizungumza na waandishi wa habari. Katikakati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin na kulia ni Cynthia Gordon, Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.

Kampuni ya Millicom leo imetangaza kuanza utekelezaji wa mpango wake wa uwekezaji katika kampuni ya Zantel, ambao utajumuisha uboreshaji wa huduma na mtandao wa kampuni hiyo.

Akizungumza baada ya mkutano wa kwanza wa bodi ya Zantel tangu Millicom iliponunua asilimia 85% ya hisa za Zantel, Mkurugenzi Mtendaji wa Milicom upande wa Africa, Cynthia Gordon, alisema maboresho hayo yatajajikita katika kuimarisha kwa huduma za simu, intaneti, pamoja ambayo yatapelekea Zantel kutoa huduma bora na ya uhakika.

'Millicom itajikita katika kuiwezesha Zantel kukuza na kuboresha ukuaji  na upanuzi wa shughuli zake hapa nchini ili kuifanya Zantel iendelee kuongoza soko la Zanzibar na kuendelea kutoa huduma zenye  ubunifu zaidi pamoja na kuongeza wigo wa kuwafikia wateja wengi zaidi’ alisema Gordon.

Kampuni ya Millicom pia imeelezea nia yake ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Zanzibar, ambayo pia anamiliki asilimia 15% ya hisa za Zantel katika kuhakikisha kampuni inakuwa msitari wa mbele katika kuwajengea uwezo na kuboresha maisha ya watu wa Zanzibar.

'Kama kampuni inayoongoza Zanzibar, ushirikiano wetu na serikali ya Zanzibar una umuhimu wa kipekee, na katika hili, Millicom itahakikisha wananchi wa Zanzibar wanawezeshwa kupitia miradi mbalimbali ya kijamii’ alisema Rachel Samren, Makamu wa Rais, Mambo ya Nje wa Millicom.

Pia akizungumza katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema kampuni ya Zantel pia itazindua mtandao wa kwanza kabisa wa 4G kwa Zanzibar ambao una lengo la kuimarisha nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika huduma za intaneti pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma za mtandao kwa wakazi wa Zanzibar.

‘Zantel itafaidikia moja kwa moja na uzoefu pamoja na utamaduni wa ubora wa Millicom, hivyo kuhakikisha Zantel inaingia katika zama mpya za kuboresha bidhaa zake na kuongeza ubora wa huduma ikiwemo huduma za kifedha kwa njia ya simu ya mkononi na kupanua maeneo ya ushirikiano katika miradi ya kijamii’ alisema Benoit.

Benoit ambaye hivi karibuni alitembelea wafanyakazi upande wa Zanzibar, amesema amejionea namna walivyo na ari ya kushirikiana na uongozi mpya wa Zantel katika kuhakikisha kampuni yao inaendelea kuongoza Zanzibar.

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Zantel pia itafanya uzinduzi wa huduma za kusisimua ikiwa ni pamoja na kupanuliwa kwa huduma za 3G na 4G na pia kuboresha  huduma za kifedha kwa njia ya simu ili kuifanya Zantel kufikia malengo yake katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Post a Comment