Tuesday, August 04, 2015

LAPF YANG'ARISHA MAONESHO YA NANENANE –DODOMA

 Mwanachama akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Bi Rehema Mkamba
 Banda la Mfuko wa Pesheni wa LAPF ambalo lipo kwenye jengo la Ofisi ya waziri Mkuu, uwanja wa Nanenane, Dodoma
Wanachama wakipata maelezo kuhusu bidhaa zinatolewa na LAPF ambazo ni uwezo wa kujichangia katika mfumo wa hiari, mkopo wa elimu, mkopo wa kujikimu, mkopo wa nyumba na fao la uzazi. 

LAPF ni mfuko bora wa pensheni Tanzania pia umeshiriki Maonesho haya ya Nanenane 2015.LAPF ipo banda la ofisi za Waziri Mkuu TAMISEMI
Katika banda hilo, LAPF tunatoa huduma zote za hifadhi ya jamii,kuu zikiwa ni;Elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania yaani tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi.

Tunaandikisha wanachama wapya wa hiari, wa kisheria na waajiri na kutoa vitambulisho hapohapo kwenye banda la LAPF
Wanachama wanapata fursa ya kuona michango yao na ya mwajairi na kupata nakala inayo onyesha michango yao Tunajibu maswali ya wanachama, kupokea maoni ya wanachama na wananchi wote kwa ujumla.

LAPF inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza kuhusu hifadhi ya jamii, kujiunga na kujionea huduma bora zilizo pelekea  LAPF kuzawadia tuzo ya mfuko bora na msimamizi na mdhibiti wa sekta  ya hifadhi ya jamii pia kupata tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa miaka mitano kwa utunzaji bora wa mahesabu ya mfuko
Karibu sana banda la LAPF.

No comments: