Zitto Kabwe Ang'uruma Ujiji, Bitale, Mahembe, Mwandiga na Kasulu Kigoma Maelfu Wajitokeza

Picha Juu ni Sehemu ya Umati Mkubwa wa Wana Kasulu Wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wa Kigoma kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe akihutubiaa Maelfu ya Wanachama wa Chadema
Sehemu ya umati wa wananchi Kasulu Jana kwenye mkutano wetu wa hadhara baada ya kikao Cha Kamati ya mashauriano mkoa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu Chadema Zitto Kabwe Akiunguruma Mbele ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Kasulu.Picha Zote na Kabwe Zitto(MB)
---
Nimehitimisha ziara yangu mkoani Kigoma kwa kufanya kikao cha Kamati ya Mashauriano ya Mkoa wa Kigoma cha CHADEMA na baadaye mkutano wa hadhara Kasulu mjini. Tumekubaliana na wananchi umuhimu wa kuendelea kuifanya Kigoma ngome ya siasa za mageuzi nchini kupitia CHADEMA. 
Nimewakumbusha wana Kigoma kwamba wao ndio mkoa wa Kwanza kukubali mageuzi nchini tangu vyama vingi.

Zitto Kabwe(MB)

Comments