Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa
juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea
jana February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.
Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia
walihudhuria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe
baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa uongozi wa juu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake jana February 27,
2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi
Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa
na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya
jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yao jana February 27, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam
alipotembelea jana February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies
Mwamunyange pia wapo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada
mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea jana February
27, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka kwenye uwanja wa sherehe
baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa uongozi wa juu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake jana February 27,
2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi
Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.Picha na IKULU
Comments