RAIS KIKWETE AZINDUA ZOEZI LA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA KARIMJEE JIJINI DAR LEO

 Rais Kikwete akiangalia kitambulisho chake baada ya uzinduzi huo.
Rais Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua rasmi zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa katika sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiwemo marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Amani Abeid Karume. Baada ya zoezi la uzinduzi, Rais Kikwete aliwakabidhi baadhi ya viongozi vitambulisho vyao vya taifa.

Naye Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Dk. Emmanuel  Nchimbi alisema ni  muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya kitaifa.
 
Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI, Mifumo ya mawasiliano ya simu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.

Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
 
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni  vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini  takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha  mpango huo kwa muda utaotakiwa.

Comments