RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI MSUMI KUWA MWENYEKITI BARAZA LA MAADILI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 26 Februari, 2013 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka huu, 2013

Comments