Rais Kikwete afungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Dodoma


8E9U7722 
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa White House uliopo katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajume wa Kamati kuu.
8E9U7730 
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum iliyofunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
8E9U7862 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina maalum kwaajili ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa White House makao makuu leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(Wapili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne kushoto), na kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula(Picha na Freddy Maro)

Comments