Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Akutana na Kufanya Mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akiwa na Naibu wake
Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) walipokutana kwa mazungumzo na ujumbe
kutoka Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje wa nchi hiyo Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani)
Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakiendelea
na mazungumzo na ujumbe huo kutoka China kuhusu masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na China. Kulia kwa Mhe. Membe ni Balozi
Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Membe akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo huku Mhe Zhai Jun na wajumbe wengine wakisikiliza
Wajumbe wa China na Tanzania kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo hayo.
Mhe. Zhai Jun, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani) na wajumbe wengine.
Mhe. Zhai Jun (katikati), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China akimsikiliza Mhe.
Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni
Mhe. Lu Youqing (kulia), Balozi wa China hapa nchini na Bi. Zhang Jing,
Mkalimani wa ujumbe huo.
Mhe. Membe na Mhe. Maalim
wakimsikiliza Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao.
Wengine katika picha ni Wajumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo hayo.
Wajumbe wengine wa Tanzania
waliokuwepo kwenye mazungumzo hayo. Kulia ni Bw. Assah Mwambene,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo.
Mhe. Membe akimsindikiza Mhe. Zhai Jun mara baada ya mazungumzo yao
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Zhai Jun.
Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo huku Mhe. Maalim akisikiliza kwa makini.Picha Zote na Tagie Daisy Mwakawago-Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
Comments