Mshindi
wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya
kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi
aliyoishikilia.
Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili.
Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).
Mshindi
wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto),
akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na
Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo
(anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)
DStv Rewards ni
sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru
wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.
Akiongelea DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice
Tanzania, Furaha Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na
hivyo amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa
ili wapate nafasi ya kuibuka washindi.
Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box
ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona
kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina
yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745
622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona "kibox".
Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma ameshinda Subscription ya
mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea
kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!
Mshindi
wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati)
akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka
R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu
akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa
kutupwa!Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza
washindi wote.
Comments