WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO WAJINYAKULIA MAHELA YA VODACOM TANZANIA

 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingw(kulia) akiongea na Mshindi kwenye simu ya mezani wakati wa Droo  ya  kuwapata washindi wa shilingi Milioni 5 na Milioni moja  katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.wanaoshuhudia kushoto kulia ni Matina Nkurlu Meneja Uhusiano,Benjamin Michael Maneja wa Huduma za Ziada na Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe,Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kulia)akionesha moja ya namba ya simu ya mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"aliejishindia kitita cha shilingi Milioni 5 ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 kila mmoja katika promosheni hiyo inayoendelea kuchezeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni Maneja wa Huduma za ziada wa Vodacom Bw.Benjamin Michael,anaefatia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bi.Chiku Salehe. Mteja anatakiwa kutuma neno"MAHELA"kwenda namba 15544 na kuweza kujishindia.zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
Maneja wa Huduma za ziada wa Vodacom Tanzania Bw.Benjamin Michael,akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajili ya kumpata mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo, ambapo wafanyabiashara ndogondogo wa Kagera na Dar es Salaam Bw.Rashid Kagombora na Adam Ramadhan wamejinyakulia  kitita cha shilingi Milioni 5 kila mmoja.

Comments