SIKU MOJA baada ya Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake
katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo
eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar
es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko
huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi
wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya
jiji la Dar es Salaam.
Pichani ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ambalo linajengwa katika ti ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba za kulala.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la
ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na
maduka, makazi na Ofisi.
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa
maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi
huo.
Naibu
Waziri
wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani katika moja
ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF Tower
ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika zitauzwa
kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika
moja ya nyumba (apartment) zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo
linaendelea kujengwa.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene akitembezwa ndani ya jengo hilo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu.
Watumishi wa PSPF wakizungumza jambo ndani ya Jengo hilo.
Awali Naibu Waziri wa Fedha,
Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba 491
za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa
kwa Wanachama wa mfukjo huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo,
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu,
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha
Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Nyumba hizo zikiwa
zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha
Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF,
Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene nje ya
moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF, kwaajili ya kuwauzia wanachama wake
kwa gharama nafuu.
Comments