Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete Watembelea Ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Picha Zote na IKULU
--
Rais
Jakaya Kikwete jana amefanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma na kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi wilayani Uvinza
mkoani Kigoma.
Rais
Kikwete alitembelea daraja hilo na kuzungumza na wananchi wa eneo jirani na
daraja hilo na kuwataka walitumie vyemka katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni
pamoja na kutumia ardhi yao kwa kilimo na si kuiuza kwa watu wengine.
Kikwete
amewaambia wakazi hao kuwa wasikubali kulubuniwa na wageni wanaokuja kama
wawekezaji na kununua maelfu ya hekta za ardhi yao.
Comments