Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
(kulia) akipokelewa na Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza,
Dk. Juma Malewa kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia kwa wakuu wa magereza
wa mikoa yote Tanzania Bara, maafisa waandamizi wa makao makuu, watumishi
raia na askari kutoka magereza mbalimbali nchini. Mfunzo hayo ya siku
nne yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali
John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ili afungue mafunzo ya jinsia
kwa maafisa magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza kabla ya kufungua
mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, John Minja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi hilo,
Deonis Chamulesile.
Maafisa Magereza wakimsikiliza
kwa makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba
ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(kulia) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko
ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta baada ya kumkabidhi taarifa
ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika Taasisi zinazotekeleza
Programu ya Maboresho ya Sekta hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(wa katikati waliokaa) akiwa na Wakuu wa Magereza ya Mikoa yote ya Tanzania
Bara katika picha ya pamoja.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments