Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiserebuka na mkewe kwenye sherehe hiyo, hoteli ya Serena juzi Jumamosi.
******************
Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu amesema kwamba kipaumbele
cha Shirika hilo kwa sasa ni kujenga nyumba za gharama nafuu nchi nzima ili
mkuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuwa na makazi bora na yenye staha kwa
maisha yao.
Akizungumza
kwenye sherehe za kuuga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, alisema kwamba
mwelekeo wa sasa wa shirika ni kuwekeza nguvu zote katika kuhakikisha makazi
bora nay a bei nafuu yanapatikana kwaajili ya wananchi wa Tanzania.
“Lengo letu kwa
mwaka huu ulioanza majuzi ni kuhakikisha tunajenga nyumba nyingi zaidi za
gharama nafuu nchi nzima ili kuwezesha watanzania wengi zaidi kumiliki makazi
bora na kuwaondolea adha ya kuyakosa makazi hayo,”alisema.
Alisema Shirika
lake katika utekelezaji wa mpango mkakati wa Shirika unaolenga kujenga nyumba
15,000 hadi kufika mwaka 2015 , Shirika hilo litahakikisha linaweka mikoani
majengo ya heshima ambayo yatakuwa kioo kwa majengo mengine yote na hivyo
kuboresha uchumi wa mikoa husika lakini pia kupendezesha mikoa hiyo.
“Tumeazimia
angalau kila mkoa tulipo tunajenga iconic building ambalo litapendezesha mji ,
lakini pia litainua hali ya uchumi ya mikoa husika kwa kuwa tukishajenga
majengo yenye hadhi na usalama wa uhakika , basi taasisi na asai mbalimbali za
kiuchumi zitanunua au kupanga katika majengo yetu na kwa kufanya hivyo uchumi
wa maeneo husika utapanda,”alisema.
Katika shughuli
hiyo, Mchechu aliwaomba wafanyakazi kuendelea kujituma pamoja na kukabiliana na
ushindani wa kikazi sambamba na kuhakikisha wanafanikiwa kuendesha maisha yao
kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya kujipatia kipato.
Alisema hivi
sasa Shirika limejiwekea mfumo wa kutathimini utendaji ambapo wale ambao
wataonekana kuwa wamefanya kazi bora zaidi watazawadiwa na wale ambao
wanaonekana kulega lega watakumbushwa na wanaoshindwa kabisa hatakuwa na budi
kuagana nao ili kusudi kuwatendea haki wanayostahili kwa kazi wanayofanya.
Dk naye Kabogo naye hakuwa mbali kusakata ngoma ya Baikoko
Wafanyakazi wakisakata rhumba
Wanaingia ukumbini
Utamu wa ngoma
Hawa vijana wanapatikana pale
Mkurugenzi Mkuu, Nehemia Mchechu akimlisha keki mke wa mfanyakazi aliyefanya kazi muda mrefu zaidi Shirikani, Bwana Mwakigosi (kushoto). Mwakigosi amefanya kazi NHC tangu mwaka 1979.
Mwenyekiti wa TAMICO, Daniel Nkya akigongesha glasi na wafanyakazi wenzake
Mkurugenzi Mkuu, Nehemia Mchechu
MC wetu Ephraim Kibonde akifanya mambo yake
Mdau Itandula Gambalagi (mwenye shati jeupe) akibadilishana mawazo na Veronica Mtemi (aliyesimama)
Mke wa Mkurugenzi Mkuu akicheza na baadhi ya wafanyakazi wake hapa ilikuwa ni katika miondoko ya kwaito.
Comments