Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Enoch Osei-Safo akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa mshindi wa shindano la shinda na Babkubwa.
Ipyana Mwakasaka akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Mkuu wa Ecobank, Enoch Osei-Safo (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari aina Hyundai Tucson ix35 lenye thamani ya shilingi milioni 65 mshindi wa shindano la Shinda na Babkubwa.
Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Umma wa Ecobank, Ndabu Swire akizungumza
wakati wa hafala ya kutoa zawadi kwa mshindi wa Shindano la Babkubwa
lililoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Ipyana Mwakasaka akijaribu kifaa
chake alichokabidhiwa mchana huu na Ecobank baada ya kuibuka mshindi
katika shindano la Shinda na Babkubwa lililoendeshwa na benki hiyo.
******
MKAZI wa Tegeta Dar es Salaam, Ipyana Mwakasaka, ameibuka
mshindi wa zawadi ya gari aina ya Hyundai Tucson ix35 lenye thamani ya shilingi
milioni 65, katika shindano la Shinda na Babkubwa, lililokuwa likiendeshwa na
Benki ya Ecobank ya jijini Dar es Salaam.
Mshindi huyo alitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wafanyabiashara Wadogo wa Ecobank, Joyce
Malai, kuhitimisha shidano la miezi sita na kusimamiwa na Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha nchini.
Malai alisema kuwa, shindano hilo lilianza rasmi Juni mwaka
jana na kudumu hadi Desemba, huku washindi wa zawadi za kompyuta mpakato
‘laptops’, vocha za manunuzi na tiketi za ndege wakipatikana, kabla ya mchakato
wa kumpata mshindi wa zawadi kuu.
“Walengwa walikuwa ni wateja binafsi, wajasiriamali, kampuni
ndogondogo na za kati (SMEs), likiwa na dhumuni la kutanua uelewa wa Watanzania
juu huduma za Ecobank, ikiwamo kuimarisha tamaduni chanya ya watu kujiwekea
akiba katika taasisi za kifedha,” alisema Malai.
Malai aliongeza kuwa, Ecobank imejipanga kuendelea
kuwaboreshea huduma wateja wake kwa mwaka huu wa 2013, sambamba na mageuzi
mengine chanya yanayofanywa na benki inayotoa huduma katika mataifa 33 barani
Afrika.
Akizungumza baada ya kupokea funguo za gari aina hiyo kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Enoch Osei-Safo, Mwakasaka aliishukuru benki hiyo
kwa kuwajali wateja na kutimiza ahadi ya kukabidhi zawadi hiyo ambayo
hakuitarajia, ingawa imekuja wakati muafaka.
“Nimefurahi kuwa mshindi na kupata zawadi ya gari la thamani
kubwa ambalo sikuwa na ndoto ya kulimiliki. Naishukuru Ecobank, huku nikiwataka
Watanzania kutumia huduma za benki hii na kuepuka utunzaji pesa majumbani ambao
ni hatari,” alisema Mwakasaka.
Comments
slipway to get the duet moving in a new management. comfortably now, if you're thought process correct you use Christian marriage counseling, tierce areas testament be given care by the attendance counsellor. almost marriages scramble through some rocky marriage is in hassle and then it is.
my web blog :: marriage counseling las vegas