Wapangaji wasio na mikataba nyumba za NHC kuondolewa

Mkurugenzi wa Usimamizi Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Hamad Abdallah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masuala ya upangaji na upangishaji, kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari

        **********************************************************************


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo tarehe 13 Februari 2013, Shirika la Nyumba la Taifa linapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa lipo katika mchakato wa kuboresha mazingira upangaji na upangishaji na leo linataka kutoa taarifa kuu mbili muhimu.

1.    Kupangishana katika nyumba za Shirika bila Kibali (Illegal Subletting)
Mwaka 2010, Shirika liliwatangazia watu waliopangishwa kwenye nyumba za Shirika kinyume cha taratibu wajitokeze ili waweze kupewa upangaji moja kwa moja na Shirika. Baadhi yao walijitokeza na walipewa upangaji.
Hata hivyo imeonekana kuna ambao hawakujitokeza kwasababu yoyote ile, Shirika sasa linawatangazia tena wajitokeze ili waweze kuhalalishwa ukaaji wao (kupewa upangaji wa Shirika). Wanaombwa kujitokeza ndani ya kipindi cha miezi mitatu (kuanzia tarehe ya taarifa hii).
Baada ya hapo fursa ya kutambuliwa haitakuwapo tena, bali watatolewa kwenye nyumba hizo na zitapangishwa kwa watu wengine.
2. Uhuishaji wa mikataba ya upangaji (Lease Renewal)
Mwaka 2006 Shirika lilifanya uhakiki wa wapangaji pamoja na kutoa mikataba mipya yenye muda maalumu baada ya kufuta ile iliyokuwa haina kikomo. Imeonekana kuna wapangaji ambao hawakujitokeza kipindi hicho,  wengine waliopewa mikataba ya muda maalumu imeshakwisha muda wake.
Shirika limefanya juhudi mbalimbali ikiwamo kuwaandikia barua za kuwakumbusha kwenda ofisi za Shirika kuchukua mikataba, baadhi wamekwenda na wengine hawajafanya hivyo na kubaki bila mikataba.
Shirika linapenda ifahamike kuwa kwa mpangaji kutokuwa na mkataba kwasababu yoyote ile ina maana kwamba hajakubaliana na masharti ya upangaji. Shirika linatoa muda wa mwezi mmoja kuanzia tarehe ya taarifa hii kwa yeyote ambaye mkataba wake umemaliza muda au hana mkataba afike ofisi za Shirika ili aweze kupewa mkataba.
Shirika linapenda kusisitiza kuwa kutokufanya hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliotolewa tachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa masharti ya upangaji na baada ya hapo wale wote ambao watakuwa hawana mikataba ya upangaji . Shirika litalazimika kuwatoa kwenye nyumba kwani watakuwa wameonyesha kuwa hawahitaji upangaji.
Shirika pia linapenda ifahamike kuwa halina mikataba ambayo haina kikomo wala mikataba ya mwezi kwa mwezi. Pia mkataba ili ukamilike lazima uwe umesainiwa na pande zote mbili yaani Shirika la Nyumba na mpangaji anayetambulika.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA


Comments

Anonymous said…
I've been browsing online more than three hours as of late, but I by no means discovered any fascinating article like yours. It is pretty price enough for me. In my view, if all site owners and bloggers made good content material as you probably did, the net might be a lot more useful than ever before.

my page :: gadgetshop.com voucher codes
My page > information technology for the health professions
Anonymous said…
Ηi, I lоg on to your blog on a regular basiѕ.
Your humoristіc style iѕ witty, κeeр doing what уou're doing!

Review my web site :: internet marketing for dummies
Anonymous said…
Aρpreciating the persistence you ρut into уour wеbsіte and detaіled
infοrmatiоn you present. It's great to come across a blog every once in a while that isn't the
ѕаme outԁated rеhаshed infoгmаtiοn.
Fantastiс rеaԁ! I've bookmarked your site and I'm
аdding youг RЅS feedѕ to my Gοogle account.


My webpаge: computershare.co.uk/careers