Makamu
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Said Arfi, akihutumia katika mkutano wa
hadhara wa Dodoma kwenye Viwanja vya Mwanga Bar na kuhudhuliwa na umati
wa watu.
---
Na Bryceson Mathias-Dodoma.
MAKAMU
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasi na Maendeleo Taifa na Mbunge wa
Mpanda Mjini, Said Arfi, amewataka watanzania kamwe wasikubali
kugawanywa, kudanganywa, kutenganishwa na kukosanishwa na Chama cha
Mapinduzi (CCM) kinachopandikiza itikadi za udini.
Arfi
alisema hayo katika Mkutano wa adhara uliofanyika katika Viwanja vya
Mwanga Bar mkoani DodomaAkihutubia maelfu ya watu ambao baadaye
walijipanga na kuwapa kadi za Chadema baada ya kuamua kuvua Magamba na
kuvaa Magwanda Arfi
alisema, awali CCM walitumia njia hiyo kwa kukiita Chama cha wanachi
CUF ni cha Ki-Islam na wakafanikiwa kukisambaratisha kwa Wakristo
kukihama.
“Baada ya
Mbinu za kukiita Chadema ni kikabila na kwamba ni cha Kikristo
kushindwa, sasa wameanza kutafuta Mbinu za kuwapotosha, kuwadanganya,
ili kuwatenganisha, kuwakosanisha, kuwaogofya, kuwatishia na
kuwapandikizia udini”.alisema Arfi akisema yeye ni M-Islamu na hajawahi
kupata hasara.
Huku
akishangiliwa na uwanja mzima Arfi alisema, yeye ni M-Islamu, hakuna
mahali ndani ya Kurani panaposema mtu aue halafu Mungu atampa kheri na
pepo, akiwa Ahera zaidi ya Laana kumuanzia hapa duniani.
Aliwashukia
Polisi na Usalama wa Taifa kuwa ifike mahali wasione aibu kusema
wameshindwa wajibu wao wa kuwalinda watanzania, jamboa alilosema kama
wameshindwa, sasa wanatakiwa wakae pembeni na
wakikaidi watalazimishwashwa na guvu ya Umma.
Mbali ya
shutuma hizo Arfi aliitaka Serikali ya CCM iwaombe radhi watanzania kwa
kuwaigiza kwenye ugomvi wa kidini, ambapo hapo awali alisema hakuna mtu
aliekuwa akiuliza habari ya kuchinja na kugombea madarakani kwa Udini,
Ukabila, Undugu, Urafiki na Upenzi.
Arfi aliiponda
CCM na Viongozi wake akisema, hivi sasa wanatumika kupoteza fedha za
walalhoi mamilioni kwa mamilioni kupigia kura ya maajabu ya Mlima
Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti, badala ya
kutumia fedha hiyo kukomesha maajabu ya mtoto kufaulu mtihani kwenda
Sekondari wakati hajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Aidha
aliwasihi watanzania wajiulize mioyoni mwao, Je kura yao imewasaidia
nini? Kama haijawasaidia basi kwa mtu yeyote waliyempa madaraka na
wajibu huo, basi waihukumu Serikali hiyo mwaka 2015 na kudai hilo
litawezekana tu kwa kuunganisha nguvu na kuing’oa CCM madarakani.
Awali Kigaila
akiwahutubia wana Dodoma kabla ya kumuachia Uwanja Arfi alisema, Kitendo
cha Spika wa Bunge Anne Makinda kuzima Hoja za Wapinzani ya James
Mbatia kuhusu Udhaifu wa Sekta ya Elimu yenye Maslahi kwa Watanzania na
ya John Mnyika kuhusu Shida ya Majiji Jijini Dar es Salaam na nchi
nzima, ingekuwa ni Arusha asingeingia bungeni wananchi wangemzuia kwa
nguvu ya umma.
Huku
akishangazwa na uoga wa wananchi hao, Kigaila aliwashukia akisema,
wakazi wa Dodoma ikifika hapo ndipo mahali huwa wanauza utu na kupoteza
haki yao ambapo watu hurudi nyuma na kujificha kwenye uchochoro wa
nyumba na Mitaa yao wakajifungia ndani.
Kigaila
alisema lakini siyo watu wa Arusha. Arusha, Waziri Shukuru Kawambwa na
Naibu wake Philip Mulugo wasingethubutu kunusa bungeni waje wawahadai
wananachi kutokana na kuwaharibia watoto wao kwa Elimu yao feki, huku
wakiwasomesha watoto wao ulaya ili waje wawatawale wa walalahoi.
Mapema Kigaila
aliwataka usalama wa taifa waweke vyombo vyao vizuri ili wamfikishie
habari na Salamu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi, sababu za
kuzuia mikutano wakati wa Bunge ambapo aliwahoji wananchi akisema,
Comments