MAANDAMANO NA MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA MWEMBEYANGA KUWAPOKEA WABUNGE WAKE WAKITOKEA DODOMA

 Picha Juu Mamia ya wakazi wa Dar es salaam walijitokeza kuunga mkono maandamano yaliyoandaliwa na chadema kupinga Uonevu wanaofanyiwa wabunge wa Upinzani Bungeni.
 Viongozi wa chadema wakiwa katika mshikamano mkubwa, wakiandamana kupinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Spika na Naibu wake dhidi ya wabunge wa Upinzani.
 Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akiwa jukwaani katika mkutano wa kulaani vitendo vya uonevu kwa wapinzani. Mkutano uliofanyika katika kiwanja cha mwembeyanga Temeke leo.
 Mbunge wa singida Magharibi-Chadema na Mnadhimu mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu akiongea kwenye mkutano uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema,John Mnyika akiongea katika mkutano.
 Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema, Godbless Lema naye akimwaga cheche jukwaani.
 Mbunge wa iringa Mjini-Chadema, Pter Msigwa akiunguruma
 
 Mbunge wa Kawe-Chadema,Halima  Mdee amesema tukianza 2014 itakula kwetu, tuanze sasa.
 Katibu mkuu wa AFP amesema chama chao kinaunga mkono chama makini kama Chadema
 Viongozi wa Chadema wakiwa Meza kuu kutoka kushoto katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa, Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe na naibu katibu mkuu Mh Zitto Kabwe.Picha Zote na CHADEMA
----
 VIONGOZI na mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana walifanya maandamano na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke, jijini Dar es Salaam ambako chama hicho kilitangaza nia ya kuandaa hoja ya kuwang’oa viongozi wa Bunge.

Hoja hiyo itawasilishwa katika mkutano ujao wa Bunge kwa ajili ya kuwapigia kura za kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kwa madai ya kukwamisha mijadala yenye masilahi ya wananchi bungeni.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Temeke Mwisho, Dar es Salaam, wabunge wa chama hicho wakiwa na uongozi wa juu, waliwataka wananchi waliohudhuria mkutano huo kujiandaa na maandamano ya kuwang’oa spika hao.Kana kwamba hiyo haitoshi, wabunge hao walitangaza namba za simu za viongozi hao wa Bunge ili wananchi wazitumie kuwashinikiza wang’oke.
Akihutubia katika mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara), Zitto Kabwe alisema Spika Makinda ameshindwa kuwajibika na hivyo anapaswa kung’olewa kutokana na kutaka kuirudisha nchi kwenye kipindi cha kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (Epa).
Akizungumzia kitendo cha Spika Makinda kuifuta Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema imefutwa kwa mbinu za CCM kuzima sauti ya wabunge wa upinzani wanaozungumzia masilahi ya wananchi.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.....>>>>

Comments