Friday, February 22, 2013

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa abwagwa Uaskofu Mkuu wa Anglikana


ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa ---- ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa ameshindwa kutetea nafasi yake ya uskofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania baada ya kushindwa na Dk Jacobo Chimeledya (56) wa Jimbo la Mpwapwa. Askofu Chimeledya ambaye anakuwa kiongozi wa sita kushika wadhifa huo nchini, aliibuka mshindi baada ya jina lake kupenya katika hatua tatu za kura. Akitangaza matokeo hayo jana jioni, Katibu Mkuu wa Anglikana, Dk Dickson Chilongani alisema kanisa hilo halina utaratibu wa kutangaza kura zilizopigwa lakini akathibitisha kuwa Askofu Chimeledya ndiye mshindi. Dk Chilongani alisema kuchaguliwa kwa Askofu Chimeledya ni utaratibu wa kanisa hilo ambalo hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....>>>

No comments:

DKT. ABBASI AKAGUA MIRADI YA UTALII PORI LA AKIBA LA PANDE, ATOA MAAGIZO YA KUKAMILIKA KABLA YA AFCON 2027

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 23, 2026, ametembelea Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaa...