Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini na
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa(Kulia)akikabidhiwa hati za kiwanja cha ekari 3 cha
kujenga hospitali ya Mama na Mtoto kutoka kwa moja wa mawakili na wakurugenzi wa kampuni ya Mawala Advocate.Sherehe za makabidhianio ziliudhuriwa na Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe
Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini na
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa akiwa na hati muda mfupi baada ya kukabidhiwa.Picha na Chadema
---
CHADEMA
ikiongozwa na kamanda Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini na
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa wamekabidhiwa kiwanja cha ekari 3 cha
kujenga hospitali ya Mama na Mtoto. Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyowahi
kuwaahidi wananchi wa Arusha katika uchaguzi wa 2010. Kiwanja hicho
chenye thamani ya dolla za kimarekanai USD300,000 sawa na Tsh
480,000,000/ kimekabidhiwa na kampuni ya Mawala Advocates
waliowakilishwa na moja ya mawakili na wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Hatua hii inamaliza propaganda na uvumi wa shutuma zilizokuwa zikienezwa
na mawakala wa CCM dhidi ya Lema kuwa amekabidhiwa kiwanja hicho na
ameandikisha kwa jina la mke wake.
Comments