Sunday, February 24, 2013

MAMA SALMA KIKWETE ACHANGISHA SHILINGI MILIONI 142.5 HARAMBEE YA MONTAGECHARITY BALL



Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar. 
 Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika hafla hiyo. 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake
Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa.
 Makofi  ya pongezi na shukurani kwa Bonge Barabarani yakipigwa.
 Mama Salma Kikwete akimkabidhi mmoja wa Wakilishi wa Kampuni ya ndege ya Flight Link cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo.

No comments: