Monday, December 07, 2015

VANESSA MDEE ANOGESHA TAMASHA LA TRUST “DIVAS ONLY” JIJINI MBEYA.

 Msanii Vanessa Mdee akitoa burudani kwa madiva wa jiji la Mbeya wakati wa Tamasha la Trust “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika jijini humo katika ukumbi wa Mtenda Sunset uliopo Soweto lengo la Tamasha likiwa ni kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa akina dada na mama wa jiji hilo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Katikati) akiwajibika jukwaani mbele ya umati wa akina dada waliojitokeza kwenye Tamasha la “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Mtenda, Sunset-Soweto jijini Mbeya. burudani hiyo ya nguvu iliandaliwa na chapa ya Trust toka shirika lisilokuwa la kiserikali la DKT International ambalo liliwakutanisha madiva kutoka sehemu mbalimbali wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee akiimba katikati ya mashabiki wake wakati wa Tamasha la “Divas Only Concert” lililoandaliwa na chapa ya Trust toka DKT International ambalo lilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. 


Mbeya TRUST imeendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hususani wakina dada katika mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya “Divas Only” ambapo kwa wikiendi hii ilikua ni zamu ya jiji la Mbeya baada ya Tamasha hilo kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Kama ilivyo ada Tamasha hilo humshirikisha Diva wa nguvu na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye alizikonga nyoyo za mashabiki wake vilivyo. Tamasha hilo liliwavutia madiva kibao kutoka maeneo ya karibu pamoja na vyuo mbalimbali vya jijini Mbeya kama TECU, Mzumbe, CBE na TIA ambapo kiingilio cha Tamasha hilo kilipangwa kuwa Tsh. 10,000/= tu. 

Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust ipo hapa kukusaidia wakati wa safari hii.

 “Kwa mara nyingine ilikuwa ni fursa nzuri ya kufurahi kwa muda tuliopata wa kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa jijini Mbeya na kufurahi na kuelimishana, tumejifunza kutoka kwa wataalamu mambo mengi na njia nyingi bora, kwamfano njia ya Kitanzi ni bora sana ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 99.9 na pia ni bora sana kwakua aina nyingi hazina vichocheo ”…

alisema Sialouise Shayo Meneja Masoko Trust. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika Tamasha letu lingine jijini Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tutafute kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!
Post a Comment