Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya Sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhuda wa ajali hiyo Bwana Julius Chacha alipotoa taarifa amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika mpaka tunaondoka eneo la tukio.
Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii
Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeungua
Hii ni njia ya mlima sekenke
Comments