Monday, December 07, 2015

MAGUFULI AIFUMUA BANDARI,MKURUGENZI MKUU,MWENYEKITI WA BODI NA KATIBU MKUU WIZARA YAUCHUKUZI OUT!!!!


KATIKA kile kinachoonekana kutotaka masikhara na uzembe uzembe katika Serikali yake, Rais Dr John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Awadh Massawe pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Prof. Joseph Msambichaka

Taarifa zinasema kuwa Dr Magufuli ameamua kufanya hivyo kutokana na uzembe uliokithiri wa baadhi ya maofisa wa bandari ambao umechangia Serikali kupoteza mabilioni ya fedha kwa kutowadai kodi wafanyabaishara waliokuwa wakiitumia bandari kama kichaka chao.


Aidha mwingine aliyekubwa na dhoruba hiyo ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.

Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli katika kasi yake ya kutumbua majipu hatimaye,amevunja bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bandari Bw.Awadhi Massawe na ameagiza wawekwe chini ya ulinzi wote na kumfukuza kazi katibu mkuu uchukuzi Bw.Shabani Mwinjaka.
Post a Comment