Tuesday, July 07, 2015

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAENDELEA KUMWAGA ELIMU KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2015


w1
Mtaalam katika   Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Rayson Nkya (kushoto) akielezea sera ya madini  kwa wananchi waliotembelea  banda la Wizara  hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
w2
Mtaalam kutoka  Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Ayoub Shija  akielezea shughuli za mgodi huo  katika banda la Wizara ya Nishati na Madini
w3
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Steven Lowoko akitoa  maelezo  juu ya  jinsi mtambo wa kufua umeme  kwa kutumia maji unavyofanya kazi kwa kutumia mfano wa mtambo huo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la  TANESCO.
w4
Afisa Mawasiliano kutoka Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI), Godwin Masabala akitoa maelezo  jinsi  taarifa za mapato  yatokanayo na rasilimali za gesi na madini zinavyokusanywa.
w5
Afisa Huduma kwa Wateja katika  Shirika la Umeme Nchini(TANESCO), Lucas Kusare (katikati) akielezea shughuli za shirika hilo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Tanesco.
w6
Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne  Shimba (kulia) akielezea shughuli za kituo hicho kwenye banda la Wizara  ya Nishati na  Madini.
w7
Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezea shughuli za uokoaji zinavyofanyika katika mgodi huo pindi majanga yanapojitokeza.
w8
Mtaalam katika   Chuo cha Madini Dodoma(MRI), Mkunde Msaky (kulia) akielezea fani zinazotolewa na chuo hicho kwa wananchi waliotembela banda hilo.

No comments: