Wednesday, July 01, 2015

UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA KOREA WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

1
Mmoja wa wafanyabishara wa nishati kutoka Korea akiangalia vinyago kwenye banda la Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
2
Afisa wa Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lucas Kusare ( wa pili kutoka kulia) akiwaonesha wafanyabiashara wa nishati kutoka Korea mfano wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji katika Banda la TANESCO kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
3
Mtaalam kutoka Idara ya Madini Mhandisi Rayson Nkya (Katikati) akimwonesha Makamu wa Rais wa Kampuni ya Energy and Minerals Resources Development Association ya Korea, Dk. Song Jae Ki (Kulia) moja ya machapisho ya Wizara ya Nishati na Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Godfrey Fweni kutoka Idara ya Madini ya Wizara hiyo.
4
Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Yusuph Msembele (Katikati) akimwonesha mmoja wa wafanyabiashara kutoka Korea (kulia, anayepiga picha machapisho hayo) machapisho ya Idara ya Nishati.
5
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Korea (Kulia) akiangalia vinyago katika banda la Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) Kushoto ni Afisa Utawala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Matiko Sanawa.
6
Washirki kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments: