Friday, July 03, 2015

NEC YATOA MWALIKO WA WAANGALIZI WA NDANI WA UCHAGUZI MKUU

download (2)

Na Jovina Bujulu
Taasisi na Asasi mbalimbali zimetakiwa kutuma maombi kwenye ya  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mkuu utatarajia kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo leo jijini Dar es salaam, imezitaka taasisi na asasi zenye nia ya kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu ujao kuwasilisha maombi yao katika ofisi ya NEC kuanzia  Julai 5 hadi Oktoba 6 mwaka huu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa waombaji wanatakiwa kuwalisha maombi yao yakiwa na anuani kamili ikiwemo ya makazi ya taasisi na asasi husika , mahali inapofanyia kazi, shughuli zake na sehemu ambayo taasisi inataka kuendeshea shughuli za uangalizi.
Mambo mengine yanayohitajika katika maombi hayo ni idadi ya wafanyakazi wa taasisi husika na taarifa zao binafsi na pia taasisi iambatanishe vivuli vya nakala cheti za usajili na Katiba ya Taasisi husika.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa Mamlaka ya kusajili waangalizi wa ndani kwa mujibu wa sehemu ya IV na V ya kanuni ya uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Uchaguzi Mkuu wa kuwamchagua  Rais , Wabunge na Madiwani  unatarajiwa kufanyika nchini kote Oktoba 25 mwaka huu.

No comments: