Friday, December 04, 2015

BENKI YA ADB YATOA MKOPO WA BILIONI 750 KWA TANZANIA KWA AJILI MIRADI MIWILI YA MAENDELEO

LI1Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi ,kulia ni mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero akitia saini wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI2Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akikabidhiana hati ya makubaliano ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI3Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi kulia akiwa na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI4Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD- MAELEZO
……………………………………………………………………………………….
Na jacquline Mrisho-maelezo
Dsm
Wizara ya Fedha na Benki ya Maendeleo Afrika(ADB) zimesaini mikataba yakuikopesha Tanzania shilingi bilioni 750 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi sekta mbili za maendeleo ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege nchini.
Mikataba hiyo imesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile kwa upande wa Tanzania na Mwakilishi wa Benki hiyo Dkt Tonia Kandiero.
Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba hiyo Dkt . Likwelile alisema kuwa katika mkopo wa kwanza utasaidia katika kuinua uchumi nchini kwa kuimarisha miundo mbinu ya barabara ya Tanzania bara na visiwani.
Dkt Servacius Likwelile aliongeza kuwa,mradi huu utapunguza gharama za matengenezo ya barabara pamoja na muda usafirishaji na ukarabati wa vyombo vya usafirishaji.
Naye Mwakilishi wa Benki Maendeleo ya Afrika Dkt Tonia Kandiero alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara kwa ajili ya kuimarisha kilimo hasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Ruvuma ambapo asilimia 90 ya watu wake ni wakulima.
Maeneo ambayo mradi huu yatakayoshughulika ni barabara ya kutoka Tabora (Pangale) hadi Mpanda na nyingine kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay kwa Tanzania Bara na kwa Zanzibar barabara itatoka Bububu hadi Mkokotoni na nyingine kutoka vijijini hadi Bitumen standadi.
Mkopo mwingine unaelekezwa katika ujenzi wa viwanja vya ndege vya Msalato kwa Tanzania Bara na Pemba kwa Zanzibar.

No comments: