Friday, December 04, 2015

MKUTANO WA 10 WA UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA ANALOGIA KWENDA DIGITALI KWA NCHI ZA SADC WAHITIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM.

MB1Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa  uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo jana. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada  ya  kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
MB2
MB3Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene (katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam. 
MB4Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi zaJumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
MB5Mada mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa  Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.Picha Aron Msigwa – MAELEZO.
Post a Comment