Monday, October 12, 2015

VOA AFRICA 54 YAFANYA MAHOJIANO NA MAMA SHUJAA WA CHAKULA , AMBAYE YUPO WASHINGTON DC KWA AJILI YA MKUTANO WA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

 Kushoto ni Mtangazaji Voice of America  wa Africa 54 Linord Moudou akiwa na Mama Shujaa wa Chakula 2014 msimu wa Tatu Bahati Muliga na Meneja Utetezi na Ushawishi kutoka Oxfam Eluka Kibona wakihojiwa kuhusiana na Shindano la Mama shujaa wa chakula na Jinsi linavyo wasaidia wakulima hasa wanawake.
Bahati Muliga(Kushoto)  Mama Shujaa wa Chakula 2014 msimu wa tatu, shindano linaloandaliwa na Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow ambapo kauli mbiu yao ni Wekeza kwa Wakulima wadogo wadogo inalipa akiwa na Meneja wa utetezi na Ushawishi kutoka Oxfam Eluka Kibona, wakiwa katika Studio za Voice of America.
Meneja wa Utetezi na Ushawishi kutoka Oxfam Eluka Kibona akielezea kwa kina Juu ya Shindano la Mmaa  Shujaa wa Chakula na Malengo ya Shindano hilo na Jinsi gani Kupitia shindano hilo na Kampeni ya Grow ambapo nia ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo hasa wanawake jinsi walivyofanikiwa, na mikakati ya Oxfam ya kuendelea kuwasaidia wakulima hao.
Mama Shujaa wa  Chakula 2014 Msimu wa Tatu Bahati Muligaakiongea na Mwandishi wa Habari wa Voice of America wakati wa mahojiano maalum, katika mahojiano hayo Bahati alielezea juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula pia Mafanikio yake makubwa aliyoyapata kupitia Shindano hilo(Video na VOA)
Post a Comment