Tuesday, January 27, 2026

DKT. KIJAJI AUNGANA NA RAIS SAMIA KUPANDA MITI







Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo tarehe 27 Januari 2027, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupanda miti  katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais. 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili ba Utalii Dkt. Hassan Abbas ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika tukio hilo la upandaji miti  wengine mbalimbali na wananchi, zoezi hilo la upandaji miti akiwa pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi, Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja na kutaka kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miti ikiwa na kauli mbiu ya “Uzalendo ni kutunza mazingira, Shiriki kupanda miti”

No comments:

DKT. KIJAJI AUNGANA NA RAIS SAMIA KUPANDA MITI

Na Mwandishi wetu, Zanzibar Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo tarehe 27 Januari 2027, ameungana na Rais wa Jamhuri...