Wednesday, March 11, 2026

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO, UWEZESHAJI WANAWAKE RIKA ZOTE









Tanzania imeshiriki mkutano uliohusu kufanikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake wa rika zote wakiwemo wazee.

Mkutano huo uliofanyika Machi 10, 2025 ni sehemu ya mkutano wa 70 wa Hali ya Wanawake Duniani (CSW 70) ulioanza Machi 09 hadi Machi 19, 2026 jijini New York nchini Marekani.

Lengo la Mkutano huo ni kuieleza dunia mafaniko ya Uwezeshaji Wanawake katika Sekta mbalimbali hasa upatikanaji wa Haki na huduma za Sheria.

Siku ya Pili ya Mkutano huo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu.



No comments:

MBUNGE WA BUNGE LA NORWAY AVUTIWA NA VIVUTIO VYA SERENGETI, AIKARIBISHA DUNIA KUTEMBELEA TANZANIA

Mbunge wa Bunge la Norway, Mhe. Himanshu Gulati , akiongozana na mwenyeji wake, Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo , ametembelea...