Saturday, July 04, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA TANO YA KUHIFADHI QUR-AN TUKUFU YALIYOANDALIWA NA TAASISI YA ISTIQAAMA, JIJINI DAR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama,  iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku. Picha na OMR
bil3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
bil5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR
bil6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Picha na OMR

No comments: