Wednesday, March 25, 2015

ZIARA YA MAFUNZO YA UJUMBE WA SERIKALI YA ZIMBABWE NCHINI

1
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Dkt. Steven James Bwana akiukaribisha ujumbe wa Serikali ya Zimbabwe katika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma Tanzania ilipofanya ziara ya Mafunzo nchini Tanzania juzi.
2
Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Richard Odongo akiwasilisha mada wakati wa Ziara ya Mafunzo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ilipoitembelea ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma nchini juzi.
3
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akiukaribisha Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo juzi.
4
Baadhi ya Maofisa wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa ulipoitembelea ofisi ya Rais-Utumishi
5
Afisa Tawala Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi (wa pili kushoto) Bw. Francis Sangunaa akiwasilisha mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo juzi.
6
Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi. Sarah Kibonde akiwasilisha mada wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe ulipoitembelea ofisi hiyo juzi.
7
Makamu Mwenyekiti wa Tume Ya Utumishi wa Umma ya Zimbabwe Dkt. M. Muchada akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Hifadhi ya Jamii nchini Tanzania (SSRA) Bi. Sarah Kibonde mara baada ya baada ya kumaliza ziara ya mafunzo katika ofisi hiyo juzi jioni.

No comments: