Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akitoa mada katika warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA) inayoendelea nchini
Mauritius.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akimkabidhi zawadi Mh. Fazila Jeewa waziri wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya waziri huyo kufungua rasmi warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na kati (ECASSA) inayoendelea huko nchini Mauritius.
Wajumbe wa warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko yahifadhi ya jamii kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia,Uganda na wenyeji Mauritius wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Fazila Jeewa waziriwa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya ufunguzi wawarsha hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki nakati (ECASSA) juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii inayoendelea huko nchini Mauritius.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha ya Uendeshaji wa Bodi ya Mifuko ya Hifadhi Jamii wakibadilisha mawazo. Wa pili kushoto ni, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA) Dk. Frederic Ntimarubusa akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Masuala ya Hifadhi ya Jamii nchini Mauritius, Fazila Jeewa kufungua warsha inayoendelea nchini Mauritius.
Comments